Mvutano wa wafanyabiashara na madalali Arusha washika kasi


Mvutano kati ya madalali na wafanyabiasha  wa jiji la Arusha umechukua sura  mpya baada ya zaidi ya wafanyabiashara elfu moja waliyopanga kwenye maduka yanayomilikiwa na jijini la Arusha  kwenye eneo la standi  ya daladala na soko la Kilombero kuunga mkono hatua ya serikali kuwapa notisi madalali  hili kuhakiki upya wapangaji wake  kuwa linalengo la kuondoa ukandamizaji  na ukwepaji wa kodi wanaofanywa na madalali hao.

Wakizungumza kwenye mkutano  wa dharura kujadili suala hilo wafanyabiashara  wamesema  madalali wamekuwa wakilipa kiasi kidogo cha kodi kwa halmashauri  na kuwapangisha watu wengine kwa fedha nyingi hivyo hatua ya serikali kutoa notisi kwa madali hili waingie mkataba na wafanyabiashara wenyewe itaondoa ufisadi huo.

Akitoa ufafanuzi juu ya mgogoro unaendelea baina ya madalali na wapangishaji katika maduka hayo,Meya wa jiji la  Arusha Calisti Lazaro amesema wameamua kuwaondoa madalali hili kudhibiti ukwepaji wa kodi uliyokuwa unaikosesha serkali mapato ya zaidi ya  shilingi bilioni mbili kwa mwaka.

JIUNGE NASI KATIKA
INSTAGRAM @Muungwanablog

YOUTUBE @Muungwana Tube

BOFYA HAPA KU-INSTALLAPP YA MUUNGWANA BLOG ILI UPATE URAHISI KUZISOMA HABARI ZOTE KWA WAKATI.
Mpya zaidi Nzee zaidi