News Alert:Jeshi la Polisi Mkoani Geita limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi katika harakati za kumkamata Lowassa

Jeshi la Polisi Mkoani Geita limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi, katika harakati za kumkamata Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Mandeleo CHADEMA Bw. Edward Lowassa, aliyekuwa amesimama kwa muda kuwasalimia wananchi katika soko kuu la Geita.

Lowassa alitumia wasaa huo akiwa njiani kuelekea kata ya Nkome wilayani Geita kumnadi mgombea udiwani wa kata hiyo kwenye kampeni za uchaguzi mdogo.

Katika sekeseke hilo baadhi ya waandishi wa habari waliokuwa kwenye tukio hilo pia walikamatwa na baadaye kuachiwa.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia