Nusura mahindi yamtoe roho

Geita. Mkazi wa Kijiji cha Buyoga Kata ya Buseresere mkoani Geita, Elias Mathias amenusurika kipigo kutoka kwa wananchi baada ya kukamatwa na mahindi mabichi aliyoiba kwenye mashamba ya wakulima wa Kijiji cha Buyonga.

Mathias alikamatwa na mahindi zaidi ya 60 analiyokiri kuyaiba kwenye mashamba hayo.

Sungusungu walimnusuru baada ya kuwazuia wananchi wasimuadhibu huku wakiwasihi wawaachie suala hilo watalimaliza kwa kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.

Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro, Japhet Madoshi alisema tukio hilo lilitokea juzi  asubuhi katika Soko la CCM baada ya wananchi kumtilia shaka Mathias

JIUNGE NASI KATIKA
INSTA
GRAM @Muungwanablog

FACEBOOK @Muungwana Blog

YOUTUBE @Muungwana Tube

BOFYA HAPA KU-INSTALLAPP YA MUUNGWANA BLOG ILI UPATE URAHISI KUZISOMA HABARI ZOTE KWA WAKATI.
Mpya zaidi Nzee zaidi