Phiri awakunia kichwa Prisons

KOCHA wa Mbeya City, Mmalawi Kinnah Phiri amesema kwamba mechi dhidi ya Prisons ndiyo ngumu zaidi kwake kuliko mchezo mwingine wowote.

Phiri anasema hayo ikiwa imebaki wiki moja kabla ya Mbeya City kumenyana na mahasimu wao wa Jiji la Mbeya, Prisons Januari 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Akiuzungumzia mchezo huo wa marudiano wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Phiri alisema huo ndiyo mchezo mgumu zaidi kwake nchini.
“Mchezo ujao wa Ligi Kuu ndiyo mgumu zaidi kwangu katika kalenda za hapa, kwa sababu unanikutanisha na wapinzani wa mji moja, Timu zinazofahamiana kwa kila kitu," alisema Phiri.

Phiri alisema hata maandalizi ya mchezo huo huwa yanakuwa tofauti kidogo na maandalizi ya kawaida ya michezo mingine, kuhakikisha Mbeya City inaendeleza ubabe kwa Prisons.

Katika hatua nyingine, Phiri, amewapongeza wachezaji wake kwa sare ya 0-0 ugenini dhidi ya Azam kwenye mchezo wa juzi usiku uliochjezwa kwenye uwanja wa Azam Complex.

“Ni sare nzuri ya ugenini dhidi ya moja ya timu ngumu katika Ligi Kuu. Kupata sare ya ugenini dhidi ya timu kama Azam ni jambo zuri kabisa, nawapongeza vijana wangu kwa kufuata maelekezo yangu vizuri,”alisema.
JIUNGE NASI KATIKA
INSTAGRAM @Muungwanablog

YOUTUBE @Muungwana Tube

BOFYA HAPA KU-INSTALLAPP YA MUUNGWANA BLOG ILI UPATE URAHISI KUZISOMA HABARI ZOTE KWA WAKATI.

Mpya zaidi Nzee zaidi