Rais Magufuli aivunja kamati ya maafa ya tetemeko la ardhi mkoani Kagera

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameivunja kamati ya maafa kagera iliyokuwa ikiratibu masuala ya maafa ya tetemeko la ardhi lilitotokea mkoani humo na kuagiza shughuli zote zilizokuwa zikifanywa na kamati hiyo zishulighulikiwa moja kwa moja na kitengo cha maafa cha ofisi ya waziri mkuu.

Rais huyo ambaye amehitimisha ziara yake ya siku mbili aliyoifanya mkoani Kagera ameivunja kamati hiyo wakati akizungumza wananchi kwenye mkutano wa hadhara ambao umefanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya Ihungo, amesema amelazimika kuivunja ili wajumbe wa kamati hiyo ambao ni viongozi wa serikali katika ngazi mkoa huo na wilaya zilizoko mkoani humo waendelee na shughuli zao za kila siku za kuwahudumia wananchi.
 
Rais huyo amekagua ukarabati wa shule ya Omumwani iliyokuwa chini ya chama cha mapinduzi ambayo ameagiza iwe chini ya serikali na amewatembelea wazee ambao amewapa msaada wa mabati na pia amekagua ujenzi wa shule ya sekondari ya Ihungo na kuiweka jiwe la msingi ambapo afisa mtendaji mkuu wa wakala wa majengo Tanzania Mhandisi Elius Mwakalinga amemueleza kuwa shule hiyo itajengwa kwenye viwango vya kuhimili hali ya matetemeko.

Kwa upande wake, waziri wa sera, bunge, kazi, vijana, ajira na walemavu, Mheshimiwa Jenister Mhagama amewahakikishia wananchi kuwa serikali itajitahidi kuziba mianya yote ya inayoweza kuchangia upotevu wa fedha zilizotolewa kwa ajili ya kukabiliana na maafa ya tetemeko lililotokea Kagera, naye Sarah Cooke balozi wa Uingereza nchini Tanzania ameipongeza jitihada za serikali ya rais Magufuli za kupambana na vitendo vya rushwa.
Mpya zaidi Nzee zaidi