Dele Alli akijipinda kuifungia kwa kichwa Tottenham Hotspur dakika ya 58 katika sare ya 2-2 na Manchester City leo Uwanja wa Etihad kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England. Bao lingine la Spurs limefungwa na Heung-Min Son dakika ya 77, wakati ya Man City yamefungwa na Leroy Sane dakika ya 49 na Kevin De Bruyne dakika ya 54
