Ujenzi Wa Daraja La Kijichi Na Tuangoma Kuanza

 Wakisaini Mkataba katikati ni Mstahiki Meya Wa Manispaa ya Ilala Bw Abadallah Chaulembo,Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Bw Nassib Mbaga na Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi CRJE Bw Zhao Yefang

   Katibu mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw Hashim Komba akiongea na Wananchi wa Kijichi kuhusu swala zima la Utengenezwaji wa Daraja hilo ili kuondoa Usumbufu wanaoupata wananchi kuzunguka Kigamboni na Kongowe wakati wa Msimu wa Masika.

 Mstahiki Meya wa Temeke Bw Abdallah Chaulembo akizungumza na wananchi wa Kijichi kuhusu ujenzi wa Daraja unaotarajia kuanza mapema Mwaka huu katika Eneo hilo

Baadhi ya Wananchi wa Kijichi wakiwa Katika Mkutano huo.

Serikali ya Manispaa ya wilaya ya Temekee na kampuni ya Ujenzi ya China CRJE  wametiliana saini mkataba wa Ujenzi wa Daraja litakalo unganisha  eneo la kijichi na Tuangoma  wilayani humo.

Akizungumza katika hafla hiyo mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Temeke   ambaye pia ni katibu tawala  Wilaya hiyo Hashim Komba  , amesema daraja hilo linajengwa ili kuondo usumbufu wanaoupata  wananchi wanaoishi  maeneo hayo kwa kuzunguka Kigamboni na kongowe wakati wa masika.

Aidha afafanua kuwa Daraja hilo litakuwa na urefu wa Mita 800 na barabara za mitaa zaidi ya kumi zenye urefu wa Kilomita 1.8   na  barabara  nyingine zenye urefu wa kilomita 84 zote zitajengwa kwa kiwango cha lami na kitapimwa viwanja zaidi ya mianane kuzunguka eneo  la mradi huo.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Ujenzi CRJE Zhao Yefang ameshukuru kupewa kazi hiyo ana ameahidi kufanya kwa viwango kama walivyo jenga Daraja la Kigamboni watahakikisha ubora na thamani ya hela vinazingatiwa na ndani ya mwaka mmoja watakabidhi Daraja hilo.

JIUNGE NASI KATIKA
INSTAGRAM @Muungwanablog

FACEBOOK @Muungwana Blog

YOUTUBE @Muungwana Tube

BOFYA HAPA KU-INSTALLAPP YA MUUNGWANA BLOG ILI UPATE URAHISI KUZISOMA HABARI ZOTE KWA WAKATI.

Mpya zaidi Nzee zaidi