Dar es Salaam. Mikoa yote iliyounganishwa kwenye gridi ya Taifa imekumbwa na tatizo la umeme kutokana na hitilafu iliyotokea katika mtambo wa kupooza na kusambaza umeme Ubungo, Dar es Salaam.
Hata hivyo Tanesco imeeleza kuwa umeshaanza kurejea katika baadhi ya maeneo.
Akizungumza na Mwananchi Digital kwa njia ya simu leo asubuhi, Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji amesema wataalam wanaendelea kushughulikia tatizo hilo na hali itarejea kama kawaida.
“Tatizo hili limetokea leo saa 12:32 asubuhi katika mtambo wa kilovolti 220 ambao ni wa kupoozea na kusambaza umeme uliopo Ubungo lakini kwa kuwa wataalam wameshagundua tatizo,” Muhaji amesema.