Serikali imejipanga kulipa zaidi ya shilingi milioni mianne kwa wahanga waliokumbwa na uharibifu wa mali zao ikiwemo mashamba uliofanywa na Tembo ikiwa kama sehemu ya kifuta machozi kwa wananchi hao waishio kuzunguka hifadhi ya wanyama pori ya Serengeti malipo ambayo yataanza kabla ya kuanza kwa bunge la bajeti mwezi juni mwaka huu.
Hayo yamesemwa na naibu waziri wa maliasili na utalii Mhandisi Ramo Makani alipofanya ziara yake wilayani Serengeti mkoani Mara na kujionea uharibifu mkubwa wa mashamba uliofanywa na Tembo hao.
Injinia RAMO MAKANI amesema baada ya wizara yake kuhakiki majina ya wanaostahili kulipwa kunichosubiriwa sasa ni kuanza kwa malipo ambayo amesema yatalipwa kabla ya kuanza kwa bunge la bajeti huku akiiagiza halmashauri wilayani humo kuanza kufanya uhakiki wahanga wengine waliokumbwa na kadhia hiyo hivi karibuni.
Kufuatia na tatizo la uhaba wa watumishi na vitendea kazi naibu wazi huyo anaelezea namna wizara yake ilivyojipanga.