Baraza la Taifa la Hifadhi ya mazingira (NEMC) limeandaa andiko kwa ajili ya kuhakikisha utunzaji wa mazingira ya mto Katuma mkoani Katavi kutokana shighuli za kibinadamu zinazoendelea katika mto huo hali ambayo pia inaliweka Ziwa Rukwa hatarini kutoweka kutokana na kupungua maji.
Akitoa taarifa hiyo kwa kaimu mkuu wa mkoa wa Katavi Salehe Mhando, Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) Bonaventure Baya amezitaja shughuli hizo zinazoharibu chanzo cha mto Katuma.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) Bonaventure ameongeza kuwa uharibifu huo mkubwa ulisababisha kukauka kwa mto Katuma na unaopeleka maji katika hifadhi ya Katavi na kusababisha viboko watano kufa na Ziwa Rukwa kupungua kwa kina cha maji. ,kutoka mita tisa mwaka 2000 hadi kufikia mita tatu mwaka 2016.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi Salehe Mhando amesema, mkoa umeshaanza kulishugulikia suala hilo kwa kuweza kubomoa vizuizi 46 vilivyokua vikichepusha maji katika mto huo na kupeleka katika kilimo cha umwagiliaji.