Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, alisema mapambano hayo sasa yatakuwa endelevu kama njia ya kukomesha biashara hiyo.
“Pamoja na kuwakamata watuhumiwa ambao wanahusishwa na biashara hii, si wao tu, pia tumewakamata hata watumiaji ili kuweza kupata maelezo ya kina ni wapi wanaponunua na nani anawauzia.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Julius Mjengi, alisema Jeshi la Polisi litaendelea na msako mkali ili kuweza kuwatia mbaroni watu wanaofanya biashara hiyo na watumiaji.
Alisema kuwa kati ya watuhumiwa hao, 14 ni ‘mateja’ ambao wameathirika kwa utumiaji wa dawa za kulevya na watano ni wafanyabiashara wa dawa hizo haramu.
VIDEO: Hii Ndio Top 10 ya Watu warefu Duniani
