Gesi yapunguza bei ya umeme

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI, DK. MEDARD KALEMANI.

NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani, amesema serikali imepata faida ya uzalishaji wa umeme wa bei nafuu kutokana na ugunduzi wa gesi asilia.

Dk. Kalemani alisema kutokana na uzalishaji huo, bei ya umeme imeshuka kutoka wastani wa Sh. 188.56 kwa uniti mwaka 2014 hadi wastani wa Sh. 125.85 kwa uniti mwaka jana sawa na punguzo la asilimia 33.26.

“Mbali na kupungua kwa bei ya umeme kwa uniti, gharama za maombi na ‘service charge’ ziliondolewa kuanzia Aprili mosi, 2016, lengo likiwa ni kupunguza gharama kwa wateja,” alisema Dk. Kalemani.

Aidha, alisema gesi iliyogundulika katika maeneo ya bahari ya kina kirefu ni futi za ujazo trilioni 47.08 na katika nchi kavu ni futi za ujazo trilioni 10.17 na kufanya jumla ya futi za ujazo trilioni 57.25 za gesi asilia.

Pia alisema kampuni ya Helium One imefanya ugunduzi wa gesi ya helium katika maeneo ya Ziwa Rukwa kwenye Bonde la Ufa ambapo kiasi kilichogundulika kinakadiriwa kufikia futi za ujazo bilioni 54.

Alisema gesi hiyo hutumika kupooza mashine za MRI scanners na vinu nuclear na pia hutumika katika `floating balloons.’

Dk. Kalemani alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Maida Hamad Abdallah, ambaye katika swali lake alitaka kujua ni aina ngapi za gesi asilia zilizogunduliwa na faida iliyopatikana.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Ujuwe Ugonjwa wa Busha

Kilimo cha Bamia