Kocha wa Tanzania Prisons Abdallah Mohamed amelalamikia ratiba ya ligi ambayo inazibana baadhi ya timu na kupelekea kupoteza mechi kutokana na kubanwa na ratiba isiyotoa fursa kwa wachezaji kupumzika.
Mohamed amesema Prison ilicheza katikati ya wiki mkoani Mbeya halafu ratiba ikawataka kucheza na Simba mwishoni mwa wiki hiyohiyo wakati Simba wao wakiwa wamepumzika vya kutosha baada ya kucheza dhidi ya Majimaji mwishoni mwa juma lililopita.
“Timu ilikuwa na uchovu, tulicheza mechi Jumatano tukasafiri kutoka Mbeya kuja Dar bila kupumzika, hiyo ndio sababu ya kupoteza mchezo,” – Abdallah Mohamed.
“Kucheza mechi Jumatano Mbeya halafu una mechi nyingine Dar Jumamosi unasafiri njiani bila kupumzika inasababisha vijana kuchoka sana, hapa tunatakiwa kurudi tena Mbeya kucheza na Kagera tarehe 15 fikiria hapo Prisons ipo kwenye hali gani.”
“Bado tunajiandaa na mapambano bado yanaendelea, tunahitaji nafasi ya nne tunaenda kuandaa kikosi ili tupate mafanikio zaidi.”
VIDEO: Chid Benz alivyowahi kushauri watu wakae mbali na Dawa za kulevya
