Wakati dunia inaadhimisha siku ya saratani hali kwa visiwani Zanzibar inaonyesha ugonjwa huo unaendelea kuwa ni miongoni mwa magonjwa tishio huku waathirika wakizidi kuongezeka.
Akizungumza na vyombo vya habari mwenyekiti wa jumuiya ya watu wenye saratani Zanzibar ambao ndio walioandaa maadhimisho hayo Dk Msafiri Marijani amesema bado kuna kazi kubwa na wananchi wengi hawajui na hawana mwamko na ugonjwa huo huku kukiwa hakuna takwimu sahihi za idadi kamili ya wagonjwa wa saratani Zanzibar na inakisiwa kuwa kwa kila mwaka wagonjwa 104 hugundulika kuwa na saratani.
Dr Marijani ambaye pia ni mtaaalmu wa uchunguzi katika hospitali kuu ya Mnazi moja amesema umefika wakati wa serikali kuchukua juhudi za makusudi kuanzisha programu maalumu za saratani na amewataka wanasiasa hasa wabunge na wawakilishi walizungumzie tatizo hili kwa Zanzibar,na naye kwa upande wake Meneja wa mipango katika jumuiya hiyo Zuhura Salehe Amour amesema jumuiya imekuwa ikihuka hatua ambapo zoezi la hivi karibuni wanawake 512 walijitokeza kuchunguzwa na watatu waligundulikana kuwa na saratani ya matiti.
Zanzibar ambayo imekuwa ikipiga hatua kubwa kukabiliana na UKIMWI na malaria lakini bado hadi sasa imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa ya ugonjwa wa saratani,kisukari na shinikizo la damu ambapo vifo vyingi vimekuwa vikiripotiwa tofauti na malaria na ukimwi.

VIDEO: Majanga katika Harusi..