Jalada La Kesi Ya Mauaji Aneth Msuya Laitwa Mahakama Kuu

Jalada la kesi ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mwenzake, Revocatus Muyela dhidi ya mauaji ya Aneth Msuya  limeitwa mahakama kuu.

Kesi hiyo, ilipaswa kutolewa uamuzi leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu anayeisikiiza lakini imeshindikana  kwa sababu jalada la kesi hiyo limeitwa Mahakama Kuu.

Hakimu Mwambapa alikuwa atoe uamuzi juu ya hoja zilizowasilishwa na upande wa utetezi pamoja na upande wa mashtaka ambapo Wakili John Malya aliomba washtakiwa hao waachiwe huru kwa sababu   hakuna hati ya mashtaka inayowashikilia washtakiwa hao mahakamani hapo.

Lakini kabla ya hakimu Mwambapa kutoa uamuzi,  ndugu wa marehemu waliwasilisha barua iliyopelekea zoezi la kusomwa uamuzi kusogezwa mbele.

Kwa mujibu wa barua hiyo wanataka hakimu ajitoe kusikiliza kesi hiyo kwa sababu hawana imani nae.

Kufuatia hivyo, mahakama kuu imeitisha jalada hilo. kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 20 mwaka huu kwa ajili ya kutolewa uamuzi.

 Erasto Msuya, ambaye alikuwa mfanyabiashara bilionea wa madini ya Tanzanite, pia aliuawa kwa kupigwa risasi, Agosti, 2015 eneo la Mijohoroni,  kando ya barabara ya Arusha – Moshi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro

Mapema hakimu Mwambapa alikuwa atoe uamuzi juu ya hoja zilizowasilishwa na upande wa utetezi pamoja na upande wa mashtaka ambapo Wakili John Malya aliomba washtakiwa hao waachiwe huru kwa sababu   hakuna hati ya mashtaka inayowashikilia washtakiwa hao mahakamani hapo.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa yeye aliiomba mahakama iwape muda ili waweze kutekeleza amri ya mahakama iliyotolewa.

Baada ya Wakili Kishenyi kuomba muda wa kutekeleza amri hizo za mahakama, Wakili Malya aliiambia mahakama kuwa amri ya mahakama ni sheria na upande wa mashtaka umekataa kutekeleza sheria hiyo, washtakiwa wanashikiliwa bila ya kuwa na hati yoyote inayowashikilia mahakamani hapo hivyo aliomba waachiwe huru.

Kishenyi alieleza kuwa siyo kwamba wameshindwa kuitekeleza amri ya mahakama ama vinginevyo, wanaomba muda na kwamba wanaweza kuiarifu mahakama kama wanakata rufaa ama la.

Washtakiwa hao kwa pamoja  wanadaiwa kumuua kwa makusudi Aneth Msuya, kwa kumchinja, nyumbani kwake, Kibada Kigamboni Mei 25,2016.

Miriam  ambaye ni mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo alikuwa mke wa aliyekuwa kaka wa Aneth, marehemu Erasto Msuya, maarufu kama bilionea Msuya.





VIDEO; USIPOCHEKA UTAKUWA MGONJWA


Mpya zaidi Nzee zaidi