Kocha Jose Mourinho amekaririwa akisema sheria zinazotumika dhidi yake ni tofauti na dhidi ya timu nyingine.Mourinho alizungumza hayo baada ya mchezo wao dhidi ya Hull City.Mourinho anaona waamuzi wanamuonea akitolea mfano tukio la kocha wa Liverpool Jurgen Klopp kumpayukia mwamuzi bila kuchukuliwa hatua.Mourinho anaona tukio hilo angelifanya yeye angechukuliwa hatua kali.
Sasa kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ameamua kuijibu kauli ya Mreno huyo.Klopp amekiri kwamba kitendo cha kumfuata muamuzi wa pembeni baada ya kipa wake Mignolet kupangua mkwaji wa penati ya Diego Costa hakikuwa kitendo kizuri.Lakini Klopp pia anaona tukio hilo halikuwa baya sana kama linavyozungumziwa.
“Inategemea na muamuzi wa pembeni,tunajua nini cha kufanya,niliona tukio lile halikuwa zuri na pia halikuwa baya sana” alisema Klopp.Klopp anaamini ni bahati tu ndio iliyomtokea.Amesema wakati anampayukia muamuzi huyo alisema ni jambo la ajabu sana ndio kwa mara ya kwanza anasikia jambo kama hilo.
“Kuna njia mbalimbili za kutuliza hisia,ilikuwa mechi ngumu na yenye hisia kali ikawa ngumu kuzuia hisia zangu,tunahangaika na hali kama hii sio kwangu mimi,au Mourinho na hata Wenger anapata wakati mgumu haswa katika mechi ngumu kama hii” aliongeza Klopp.
Klopp alimalizia kwa kusema anajitahidi sana kukabiliana na masuala kama hayo.Lakini hajui kwanini Mourinho amemuongelea yeye na amewambia waandishi wakamuulize Mourinho kwanini kamzungumzia yeye.