Kocha Azam atema cheche, aita Azam kushambulia zaidi kuliko kujilinda

KOCHA WA AZAM FC ,ARISTICA CIOABA.

SIKU chache baada ya kupata kibali cha kufanya kazi nchini,Kocha wa Azam FC ,Aristica Cioaba , ameweka wazi kuwa anataka timu hiyo icheze soka la kushambulia zaidi kuliko kujilinda.

Cioaba alisaini mwezi uliopita kuifundisha Azam lakini alishindwa kuanza kazi kutokana na kuchelewa kupata kibali cha kufanya kazi nchini.

Kocha huyo juzi usiku aliiongoza kwa mara ya kwanza timu hiyo kwenye mchezo wa kirafiki dhidi Red Arrows ambapo Azam iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Cioaba, alisema ameanza kazi ramsi na anataka kuona Azam wanacheza soka la nguvu na kushambulia muda wote.

“Napenda zaidi soka la kushambulia, sipendi kuona timu yangu ikiwa nyuma ikicheza zaidi soka la kujilinda, ," alisema Cioaba.
Hata hivyo, alisema ili timu hiyo icheze anavyotaka inahitaji muda kukamilisha anachokitaka.

"Tutaenda hatua kwa hatua, Azam ni timu nzuri na inawachezaji bora na bahati nzuri nimewaona mechi nyingi ninaimani tutafanikiwa kwa hili," aliongezea kusema Cioaba.

Azam kwa sasa inajiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui utakaochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku.
Mpya zaidi Nzee zaidi