Mabadiliko ya Uongozi Somalia Kibarua Kigumu Chamkabili Rais Mpya

Kiongozi mpya wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo anakabiliwa na kibarua cha kuhakikisha kwa kusaidiana na jeshi la kulinda amani la Umoja wa Afrika AMISOM, analimaliza kundi la kigaidi la Al shabab ambalo linakadiriwa kuwa na wafuasi kati ya 7,000 na 9,000 ndani na nje ya nchi.

Ugaidi nchini Somalia umesababisha maelfu ya raia wa nchi hiyo kukimbilia nchini Kenya na nchi zingine duniani.

Rais huyo mpya wa Somalia, anatarajiwa kukabiliana na changamoto za kiuchumi, ugaidi, mivutano ya kisiasa kati ya koo mbalimbali na uhaba wa chakula katika nchi hiyo.

Uchumi wa taifa la Somalia, umeendelea kuyumba hasa kwa sababu ya ukosefu wa uwekezaji na serikali kutumia kiasi kikubwa cha fedha kidogo inachopata katika masuala ya usalama kwa msaada wa nchi za nje.

Pamoja na hilo, ufisadi nchini humo umesababisha uchumi kushuka kwa kiwango kikubwa kutokana na kupotea kwa kiasi kikubwa cha fedha.

Ripoti ya mwaka uliopita iliyotolewa na Shirika la Transparency International, ilieleza kuwa Somalia ndio nchi inayoongoza kwa ufisadi duniani, sababu kubwa iinayotajwa kusababisha hali hiyo ni nchi hiyo iliyo kwenye eneo la pembe ya Afrika, kukosa taasisi za kukabiliana na tatizo hili.
Mpya zaidi Nzee zaidi