Mabeyo aapishwa kuwa Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi

Dar es Salaam. Rais John Magufuli  leo amemuapisha Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Jenerali Mabeyo aliteuliwa na Rais Magufuli Alhamisi iliyopita kushika wadhifa huo baada ya Jenerali Devis Mwamunyange kustaafu.

Jenerali Mabeyo alikuwa Luteni Jenerali kabla ya kupandishwa cheo kuwa Jenerali.

Kabla ya kuapishwa Jenerali huyo, Rais John Magufuli alimvalisha Luteni Jenerali Venance Mabeyo cheo kipya na kuwa Jenerali.

Pia, Rais Magufuli amemuapisha Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Luteni Jenerali James Mwakibolwa akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Mabeyo.

VIDEO: Wanaume 10 wazuri zaidi Duniani 2016/2017


Mpya zaidi Nzee zaidi