Majina wavuvi haramu yakabidhiwa


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amekabidhi majina 21 ya vinara wanaojihusisha na uvuvi haramu kwa vyombo vya ulinzi na usalama yakiwamo mawili ya viongozi kwa vyombo hivyo.

Akiwa kwenye ziara ya kawaida ya kukagua miradi ya maendeleo, katika wilaya hiyo (leo Jumatatu mchana) eneo la Mbweni  kuzungumza na wananchi na kusikiliza kero zao amesema amezindua rasmi vita dhidi ya wavuvi haramu.

Amesema amekabidhi majina hayo kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya uchunguzi na ilibainika wahusika wachukuliwe hatua za kinidhamu ikiwamo kupelekwa mahakamani.

"Nimezindua rasmi vita dhidi ya uvuvi haramu, sambamba na hilo natoa maagizo ya kufanyika msako kuwakamata wale wote wanaomiliki nyavu hizo kinyume cha sheria."



Mpya zaidi Nzee zaidi