Martin Kadinda Na Marafiki Wa Wema Washinda Mahakamani Huku Akisema Yeye Sio Meneja Wake Msanii Huyo Kwa Sasa

  Aliyekuwa meneja wa wema Martin Kadinda akiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam  pamoja na wanasheria

Mbunifu wa mitindo maarufiu nchini, Martin Kadinda amesema kuwa yeye sio meneja wa msanii Wema Sepetu kwa sasa bali amefika mahakamani hapo kama rafiki wa karibu wa msanii huyo.

Kadinda amesema hayo katika maongezi maalum na mwandishi huyu  juu ya uhusiano wake na Wema Sepetu kwa sasa hasa mara baada ya kuhusishwa na tuhuma za matumizi na uuzwaji wa dawa za kulevya.

“Kwa sasa mie sio meneja wa Wema.K wa sasa mimi ni rafiki yangu tu wa karibu hivyo nimeamua kuja hapa kwa ajili ya kujua rafiki yangu amefikia wapi katika kipindi hiki ambacho anapitia magumu” amesema Kadinda

Amesema  kuwa yeye kwa sasa anaendelea na biashara yake ya kushona suti tu hili aweze kujipatia ugali wake wa kila siku na sio kujihusisha na makundi ambayo sio sahihi.

Kadinda na marafiki kadhaa wa Wema wameonekana mahakamani hapo wakisubiri kwa hamu kumuona rafiki yao anafikishwa hapo lakini hakufikishwa kama ilivyoelezwa awali.

  Baadhi ya marafiki  wa Wema Spetu wakiwa wamesimama kusubiri msanii huyo kuletwa mahakamani

 Jike Shupa na wenzie wakiwa wamekata tamaa mara baada ya kuambiwa Wema haletwi mahakamani






VIDEO; TOP 10 YA VIUMBE HATARI DUNIANI

Mpya zaidi Nzee zaidi