Matumla bado yupo ICU, Ni baada ya Kipigo cha Mfaume

Bondia Mohammed Matumla, bado amelazwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi (ICU).
Matumla alipigwa na Mfaume Mfaume katika raundi ya saba katika pambano lisilo la ubingwa lililofanyika juzi.

“Labda anaweza kutoka leo hii, au kesho. Lakini hali yake inaendelea vizuri na kuna matumaini,” alisema Rashid Matumla ambaye ni baba mzazi wa Mohammed.

“Lakini kweli tunahitaji msaada, kuna mambo mengi yanatakiwa hasa suala la kulipia," aliongeza Matumla aliyewahi kuwa bingwa wa dunia.



VIDEO: Wanaume 10 wazuri zaidi Duniani 2016/2017

Mpya zaidi Nzee zaidi