Sumbawanga. Wazazi katika Halmashauri ya Sumbawanga walioamua kukaa nyumbani na watoto waliofaulu sekondari huenda wakafikishwa mahakamani iwapo hawatawapeleka shuleni.
Wanafunzi 223 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika halmashauri hiyo hawajaripoti shuleni.
Kutokana na hali hiyo, uongozi wa halmashauri umewataka wazazi na walezi wao kuwapeleka shuleni haraka iwezekanavyo kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yao, ikiwamo kufikishwa mahakamani.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Nyangi Msemakweli ametoa agizo hilo na kusema wanafunzi hao ni kati ya 2,580 waliochaguliwa kujiunga na elimu sekondari.
Amewataka wazazi na walezi kuwapeleka shuleni watoto wao kabla mwezi huu haujaisha, kinyume na hilo alisema watasakwa popote walipo na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Amesema baadhi ya wazazi huwaozesha watoto wao wanapomaliza elimu ya msingi na wengine huwakataza wa kiume kujiunga na sekondari ili kuwatumia katika shughuli za uzalishaji mali kupitia kilimo na ufugaji.
Ofisa Utumishi wa halmshauri hiyo, Deodatus Kangu amesema kuna upungufu wa madawati 4,235 na lengo lilikuwa kuandikisha wanafunzi 30,000, lakini kuna ongezeko la watoto zaidi 7,500 hivyo wamejipanga kwamba, ifikapo Machi changamoto ya upungufu wa madawati hayo iwe imetatuliwa.