Waziri mkuu mheshimiwa Kassim Majaliwa amesema serikali iko tayari kutafuta namna na kupata sukari ili kudhibiti kupanda kwa bei kwa kushirikiana na viwanda vya ndani ikiwa ni mkakati wa kuvilinda kwa lengo la kuviwezesha kuongeza uzalishaji nchini.
Akijibu maswali ya papo kwa papo, mheshimiwa Majaliwa amewahakikishia wananchi kuwa hakutakuwa na tatizo la uhaba wa sukari nchini na kusisitiza kufikia mwezi wa tatu mwaka huu viwanda vyote vinaweza vikawa vimefikia malengo ya uzalishaji.
Katika kipindi hicho cha maswali ya papo kwa papo, kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Mhe Freeman Mbowe amejikuta katika wakati mgumu baada ya maswali alilouliza kuambiwa si ya kisera.
Katika hatua nyingine serikali imeuondoa mswada wa sheria ya madaktari,madaktari wa meno na wataalamu wa afya shirikishi baada ya kutokea upotoshaji.
Wakizungumza na ITV baadhi ya wabunge wamekuwa na mtazamo tofauti kuhusu kuondolewa kwa mswada huo huku idadi kubwa ikitaka serikali kuwa makini kabla ya kuwasilisha miswada bunge ili kufanikisha kazi za bunge.

ANGALIA VIDEO POMBE SIO CHAI