TAKUKURU mkoani Mara imewafikisha maafisa wawili wa mahakama ambao ni hakimu wa mahakama ya mwanzo

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Mara imewafikisha maafisa wawili wa mahakama ambao ni hakimu wa mahakama ya mwanzo kitaji iliyopo manispaa ya musoma BW. SWALALA MATHAYO na karani wa mahakama hiyo BW. CHARLES MASATU kwa tuhuma za kudai na kupokea rushwa ya shilingi laki mbili (200,000) kinyume na kifungu cha sheria ya kuzia na kupambana na rushwa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mkuu wa takukuru mkoani Mara BW. HOLLE MAKUNGU anaelezea mazingira yaliyopelekea watuhumiwa kukutwa na hatia hiyo.

BW. HOLLE MAKUNGU amesema chanzo cha madai ya rushwa kimetokana na hakimu wa Mahakam ya mwanzo Bw. SWALALA MATHAYO kutoa hukumu ya miaka miwili jela kwa BI. MAGDALENA ALOYCE aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya jinai NAMBA CC1072/2016.
kutokana na matatizo aliyokuwa nayo ya kufungwa akiwa na mtoto wa miezi kumi gerezani huku mtoto mwingine akiachwa nyumbani bila ya uangalizi ndugu wakaona ni suluhu kuomba ruksa ili mfungwa huyo apewe kifungo cha nje.

Lakini wakati mama mzazi akifuatilia taratibu za mwanae kutolewa gerezani na kupewa kifungo cha nje likabakia suala la kuwekewa saini na hakimu wa mahakama ya mwanzo bw. SWalala ambaye alikataa kufanya hivyo huku hakimu huyo na karani wa mahakama hiyo wakimtaka mama wa mfungwa huyo kutoa rushwa ya shilingi laki mbili huku wakijua fika kufanya hivyo ni kwenda kinyume cha sheria.

Kesi hiyo namba CC 35/2017 imefikishwa mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Musoma BW. RICHARD MAGANGA na mwendesha mashtaka wa TAKUKURU wakili Bw. MARSHAL MSEJA hata hivyo washtakiwa hao walikana mashtaka na yao na wapo nje kwa dhamana hadi March 21 mwaka huu.





VIDEO: MAISHA YA SAMATTA NA CHAKULA ANACHOKIPENDA ZAIDI

Mpya zaidi Nzee zaidi