Dar es Salaam. Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe yupo nchini Kenya kwa ziara ya ukaguzi wa miradi ya Benki ya Dunia(WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).
Taarifa iliyotolewa na ofisi ya kiongozi wa chama hicho leo Jumatatu mchana imeeleza kuwa ziara hiyo ni sehemu ya kazi za mtandao wa wabunge wa IMF na WB.
"Katika ziara hii kuna jumla ya wabunge 25 kutoka nchi mbalimbali duniani. Tanzania inawakilishwa na Mbunge wa Kigoma Mjini na Mbunge wa Sikonge, Joseph Kakunda."
Imeeleza kuwa katika ziara hiyo wabunge wanakagua miradi mbali mbali inayotekelezwa na mashirika hayo na namna gani miradi hiyo inachochea maendeleo ya nchi husika.
