Wabunge Uingereza wapitisha mswada wa kujitoa EU

Wabunge nchini Uingereza wamepitisha mswada wa kujitoa Umoja wa Ulaya.

Wabunge wamepiga kura na kumpa Waziri Mkuu Theresa May mamlaka ya kuanza harakati za kujitoa Umoja wa Ulaya.

Muswada huu umepigiwa kura na kupitishwa kwa kura 494 huku wabunge wengine 122 wakiwa wamekataa.

Ni dhahiri kuwa Uingereza haina haja ya kuendelea kuwa katika EU.

Hata hivyo maamuzi haya yatapelekwa katika Bunge kuu la Uingereza kwa ajili ya kutoa uamuzi wa mwisho.
Mpya zaidi Nzee zaidi