Wajumbe wa kamati ya nishati na madini na mbunge wa simanjiro wafanya ziara katika maduka ya tanzanite, arusha.

 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mbunge wa Simanjiro, wakitembelea baadhi ya maduka yanayouza madini ya Tanzanite jijini Arusha

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mbunge wa Simanjiro, Mhe.James Millya, wametembelea baadhi ya maduka yanayouza madini ya Tanzanite jijini Arusha ili kujionea shughuli za biashara na uongezaji thamani wa madini hayo zinavyofanyika.

 Ziara hiyo ni moja ya majukumu waliyopanga kuyafanya jijini Arusha, jukumu kuu likiwa ni kushuhudia jinsi Mnada wa Pili wa Kimataifa wa Madini ya Tanzanite unavyofanyika katika kituo cha Jemolojia jijini Arusha.

Moja ya duka lililotembelewa na Wabunge hao ni The Tanzanite Experience ambalo hujishughulisha na kukata Tanzanite ili kuiweka katika maumbo mbalimbali na kuing’arisha. Duka la The Tanzanite Experience pia hutoa elimu bure kwa wanafunzi na wageni mbalimbali kuhusu madini ya Tanzanite ikiwemo historia yake.

 Ndani ya duka hilo pia kumejengwa mgodi wa mfano wa Tanzanite ambao hutumika kutoa elimu kwa wageni mbalimbali kuhusu shughuli za uchimbaji wa Tanzanite.

Baadhi ya Wajumbe waliofanya ziara hiyo ni pamoja na Mhe. John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini (CHADEMA), Mhe. Mwantakaje Juma Mbunge wa Bububu (CCM) na Mhe. Dunstan Kitandula Mbunge wa Mkinga (CCM).
Mpya zaidi Nzee zaidi