Wananchi wafanya maandamano kupinga ripoti ya Umoja wa Mataifa Burundi

Maandamano ya kuunga mkono serikali yamefanyika mjini Bujumbura  kupinga ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu.

Mwanzoni mwa juma shirika la kimataifa la haki za binadamu na shirika la kutetea haki za binadamu nchini Burundi ITEKA kwa ushirikiano yalikemea mauaji, unyanyasaji dhidi ya wanajeshi waliozuiliwa na kudaiwa kuwa jamii ya kitusi.

Maandamano ya kuunga mkono serikali yalifanyika Jumamosi kupinga ripoti hiyo iliotolewa.

Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa inatuhumu serikali ya Bujumbura kukiuka haki za binadamu.

Vijana wa chama tawal nchini Burundi waliandamana kupinga ripoti hiyo mjini Bujumbura na kusema kuwa nia ya ripoti hiyo ni kuchafua serikali iliopo madarakani.




VIDEO: Unaujua Uchungu wa Mke? Cheki hii ya Mau Fundi

Mpya zaidi Nzee zaidi