Benin yajadili rais kuongoza kwa muhula mmoja

Rais wa taifa hilo Patrice Talon alisema kuwa atajaribu kubadili katiba hiyo wakati wa kampeni ya uchaguzi mwaka uliopita.

Bunge nchini Benin limekuwa likifanya mjadala kuhusu marekebisho ya katiba ikiwemo kupunguza muda wa rais kuongoza hadi muhula mmoja wa miaka sita.

Kwa sasa rais anaweza kuongoza kwa mihula miwili ya miaka mitano kila mmoja.

Lakini pendekezo hilo linakabiliwa na utata.

Vuguvugu moja la upinzani lilifanya mgomo mbele ya bunge likisema kuwa raia wanafaa kupewa fursa ya kujadili mabadiliko hayo.

Nchini Benin marekebisho ya kikatiba yanaweza kuidhinishwa kupitia kura ya maoni ama wingi wa kura bungeni.

Rais wa taifa hilo Patrice Talon alisema kuwa atajaribu kubadili katiba hiyo wakati wa kampeni ya uchaguzi mwaka uliopita.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Ujuwe Ugonjwa wa Busha

Kilimo cha Bamia