Rais wa Somalia, Mohamed Farmajo atangaza janga la njaa kama maafa ya kitaifa. Aitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka.
Katika taarifa iliyotolewa jana na Ikulu ya Somalia, Rais Farmajo amesema, kuna wajibu wa kuchukuliwa hatua za dharura za kibinadamu katika maeneo yote yaliyoathiriwa na ukame.

