Jeshi la polisi Zanzibar limethibitisha kwa maofisa wake watano wanatuhumiwa kuhusika na uletaji,uingizaji na usambazaji wa madawa ya kulevya na tayari maofisa hao wanashugulikwa katika ngazi za juu la jeshi hilo nchini.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa jeshi la polisi Kamisheni ya Zanzibar Kamishna Mkuu CP Hamdan Omar Makame wakati akizungumza na maofisa na askari wa mikoa mitatu ya Unguja kuelezea hali ya operesheni ya vita ya dawa za kulevya na udhalilshaji wa wanawake na watoto ambapo amesema Polisi ndio wanatakiwa kuwa wasimamzi wa sheria na kuwa mstari wa mbele hivyo jambo hilo halikubaliki na taratibu za kisheria zimeshanza dhidi ya maofisa hao watano wanotuhumiwa kuhusika kwa njia zote.
CP Hamdan Omar Makame ambaye amewanyoshea kidole askari ambao wanazipinda sheria kwa makusudi wakati wanapoona uhalifu umefanyika waache na sheria ifuatwe na watakaobainika watatimuliwa kwa mujibu wa sheria huku akitangaza kuanza rasmi oparesheni maalum inayowashirikisha jeshi la polisi,afisi za waendesha mashataka na mahakama kuu katika kupambana na vitendo vya udhalilishaji na tayari mahakimu na majaji wameshateuliwa kusimamia kesi hizo kuanzia leo na wanatarijia kuwepo na kuanza kwa kesi 25.
Hatua hizo za jeshi la polisi ambazo zinapaswa kuungwa mkono na jamii zinakuja huku pakiwemo na msukumo mkubwa wa serikali kutaka polisi na vyombo vya ulinzi na usalama kuhakiksiha kwa nguvu zote wanakomesha vita dhidi ya dawa za kulevya na udhalilishaji Kisiwani Zanzibar.