kuvaa jeans kwenye vikao

Madiwani jijini Tanga waliokuwa wakivaa suruali aina ya jeans kwenye vikao vya baraza wanalazimika kuachana na nguo hizo baada ya Meya wa jiji hilo, Mustafa Mhina kupiga marufuku uvaaji wa mavazi hayo.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani Jumanne hii, Mhina alisema viongozi hao hawaruhusiwi kuvaa suruali hizo na mavazi mengine ambayo hayana staha.

Aidha Mhina amewataka madiwani kuvaa majoho na kofia na kwamba ambao hawatafuata utaratibu huo watatolewa nje ya mkutano.
Mpya zaidi Nzee zaidi