Sababu ya ngozi kuwa na mafuta hutokana na na tezi za
sebaceous na kuzalisha mafuta zaidi ya kiwango ambacho ambacho
kinatakiwa. Lakini licha ya tezi hizo aina za sebaceous kuzalisha
kiwango cha mafuta kwa wingi, zipo pia sababu nyingine ambazo zinafanya
ngozi kuwa na mafuta ambazo kama ifuatavyo.
- • Kurithi.
- • Lishe.
- • Kiwango cha homoni mbalimbali mwilini.
- • Ujauzito.
- • Baadhi ya vipodozi .
- • mabadiliko ya hali ya hewa hasa joto.
Na madhara ambayo yanatokana na ngozi yenye mafuta ni
kwamba, ngozi huweza kutengeneza ngozi yenye tabaka lisiloisha vipele
pamoja na chunusi kwa muda mrefu.
Baada ya kuona baadhi ya sababu na athari ya ngozi kuwa mafuta, sasa tuangalie namna ya kutunza ngozi zenye mafuta:
1. Ngozi yenye mafuta inahitajia kusafishwa vyema kwa maji
ya moto na sabuni ili kuzuia vinyweleo visizibwe na mafuta. Lakini
Jitahidi kuitunza vyema ngozi yako na kuisafisha vizuri. Jaribu kuosha
uso mara mbili au mara tatu kwa siku. Usioshe mara nyingi kwani kufanya
hivyo huufanya uso kutoa mafuta zaidi.
3. Epuka kutumia vipodozi ambavyo huifanya ngozi yako
ipoteze maji au kukauka. Kwani husababisha sehemu ya juu ya ngozi
inyauke, na hivyo kusababisha mafuta kuziba vinyweleo na kupelekea
kutokea kwa chunusi ambazo zitaufanya mwili kuwa na mafuta.
4. Chagua kile unachosafishia kwa makini, jiepushe kutumia
cream nzito nzito au vifaa vugumu wakati wa kuosha uso wako. Ni bora
utumie sabuni za kawaida zisizokuwa na madawa. Unaweza kutumia lotion ya
kuua bacteria au sabuni zisizo na dawa nyingi (lightly medicated), au
sabuni zenye madini mbalimbali. Ni bora usioshe au kutumia lotion au
michanganyiko yenye alkoholi.
5. Lakini pia unashauriwa ya kwamba hakikisha unatumia mafuta ambayo yametengenezwa kwa ajili ya ngozi yenye mafuta.
Endapo utayazingatia hayo mwili wako utakwenda kuwa katika hali ya ubora zaidi, na kufurahia ngozi isiyo na kasoro.