Mbwana Samatta ametajwa kwenye mtandao huu mkubwa

Baada ya ushindi wa goli 2-5 wa KRC Genk dhidi ya wenyeji wao KAA Gent katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora wa michuano ya UEFA Europa League, jina la mtanzania Mbwana Samatta limezidi kuingia kwenye headlines.


Mbwana Samatta katika ushindi wa 5-2 wa timu yake alifanikiwa kufunga magoli mawili dakika ya 41 na 72, Samatta alifunga goli la kwanza baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Jean Boetius na goli lake la pili ambalo la tano kwa timu yake alifunga kwa kutumia vizuri pasi ya nahodha wake Thomas Buffel.

Mpya zaidi Nzee zaidi