SERIKALI imezuia shughuli za uchimbaji wa madini ya vito kwenye Mto Muhuwesi wilayani Tunduru mkoani Ruvuma hadi hapo taarifa za kitaalamu zitakapotolewa baada ya kukamilika kwa tathmini na ukaguzi.
Agizo hilo lilitolewa jana wilayani humo na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alipofanya ziara kwenye mto huo ili kuona hali ya eneo husika kutokana na ajali iliyosababisha kifo cha mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Kanje Ally na majeruhi mmoja ambao waliingia na kuanza kuchimba ndani ya mto.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisa Madini Mkazi wa Wilaya ya Tunduru, Fredrick Mwanjisi, zaidi ya watu sita walivamia eneo hilo la mto kufanya shughuli za uchimbaji wa madini kinyume cha taratibu kutokana na kutokuwa na vibali vilivyowaruhusu kufanya shughuli ya uchimbaji katika eneo hilo.
Taarifa hiyo ilieleza kwamba shughuli za uchimbaji wa madini ndani ya Mto Muhuwesi zilisimamishwa tangu mwaka 2014 kutokana na pingamizi kutoka kwa Mamlaka ya Bonde la mto Ruvuma na Bonde la Kusini kwa kuzingatia Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Namba 11 ya mwaka 2009 na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira namba 20 ya mwaka 2004.
Kutokana na taarifa hiyo na baada ya kujionea hali halisi na kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo pamoja na viongozi wao, Waziri Muhongo aliagiza kusitisha haraka shughuli zote za uchimbaji madini kwenye mto huo hadi hapo taarifa ya tathmini ya athari ya shughuli ya uchimbaji kwa mazingira ya Mto Muhuwesi itakapokamilishwa na kuwasilishwa na wataalamu kutoka Mamlaka ya Bonde la Mto Ruvuma, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Wizara ya Nishati na Madini.
Ili kuhakikisha suala hilo linapata ufumbuzi wa haraka, Profesa Muhongo ametoa miezi mitatu kwa wataalamu kutoka mamlaka hizo wawe wamewasilisha taarifa hiyo kwake na kwa uongozi wa Wilaya ya Tunduru.
“Tarehe 30 Mei, 2017 wataalamu watakaohusika na ukaguzi wanatakiwa kuwasilisha taarifa yao kwa Mkuu wa Wilaya bila kukosa; hatuwezi kuendelea kukaa kimya,” alisema Profesa Muhongo, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na wizara yake.
Akisisitiza kuhusu agizo hilo la kusimamisha uchimbaji ndani ya mto, alibainisha kwamba kwa uzoefu alionao hajawahi kuona taifa lolote duniani likifanya shughuli za uchimbaji wa madini kwenye mito, lakini alisema anatoa muda kwa wataalamu husika kufanya majadiliano na kukagua athari za shughuli za uchimbaji wa madini kwenye mto huo.
Vilevile aliziagiza Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Nyasa, Songea na Ofisi ya Ofisa Madini Mkazi, Tunduru kuandaa orodha ya leseni zote kwenye wilaya inayobainisha leseni zinazofanyiwa na zisizofanyiwa kazi na kuikabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru ili kuruhusu wenye kuhitaji wayaombee leseni.
“Kuna wachimbaji walipewa maeneo lakini hawayaendelezi, wanastahili kunyang’anywa ili yakabidhiwe kwa vikundi vilivyo tayari kufanya uchimbaji,” alieleza.