Beth Battista ameiambia BBC kwamba hakusita kutoa figo yake baada tu ya kusikia jitihada za Lyla za kutafuta figo kwa muda mrefu.
Mwalimu huyo, ambae pia ni mama wa watoto wawili, amesema alisikia juu ya hali ya Lyla baada ya mamake kuweka taarifa za mwanawe katika mtandao wa Facebook.
Mwaka mmoja uliopita, Lyla alipatikana na tatizo la figo ambapo alitakiwa kusafishwa damu kwa saa kumi na mbili kwa siku.
