Peter Michael akikagua Shughuli wa Ujasiriamali Wilayani Misungwi

Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Misungwi Peter Michael (Kulia) akikagua Shughuli za Ujasiriamali katika baadhi ya Vikundi vya Akinamama wakazi wa Misungwi wakati wa Maashimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambapo alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda aliyekuwa Mgeni Rasmi.

 
(kulia) Rachel Shigela Mwenyekiti wa Kikundi cha Akinamama cha Ngudama kinachotengeneza Majiko Sanifu, Masufuria ya kupikia,Mitungi ya Maji,Chupa ya Chai, Vyombo mbalimbali vya Udongo wa Asili.

Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Misungwi amewataka Akinamama na Wananchi wote Wilayani humo kuanzisha Kilimo cha mazao ya mbogamboga ya Nyanya,na Matunda kwa lengo la kuwekeza katika Viwanda Vidogo, vya Kati na Vikubwa vya usindikaji ili kiongeza kipata cha Familia na kuinua uchumi Wilayani humo na taifa kwa ujumla.

Amewataka pia kujikita zaidi katika Vikundi vya kuzalisha Mali na kukuza mitaji yao kwa kufanya mabadiliko ya kibiashara kwa kufanya Utafiti,uchambuzi wa kina ili kufahamu bidhaa zinazotakiwa na wateja /walaji na masoko husika kulingana na mahitaji ya wakati huo.    

Kaimu Katibu Tawala huyo,aliwasisitiza Akinamama Wilayani Misungwi kutumia na kwa Vitendo Kauli Mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani,isemayo ,Tanzania ya Viwanda:

Wanawake ni Msingi wa Mabadiliko ya Kiuchumi,hivyo Wan awake hawana budi, kujijengea Kiuchumi kupitia fursa mbalimbali zilizopo kwa kupata mitaji ,mikopo yenye masharti na riba nafuu na kuanzisha Biashara ndogondogo na kuimarisha Vikundi vya ujasiriamali vilivyopo badala ya kuwa wasindikizaji tu na baadaye kunufaika na Viwanda vitakavyoanzishwa.

Aliwasihi Wananchi kuondokana na tamaduni, desturi na mila potofu zilizokuwepo za kutosomesha watoto wa kike na Wanawake kutopewa nafasi kwenye ngazi mbalimbali za maamuzi na suala la umiliki wa Ardhi mambo ambayo yamekuwa yakitokea katika baadhi ya makabila na jamii yetu, na kuomba kuachana na desturi hizo na kuweka mipango na mikakati endelevu na kutatua changamoto zitakazojitokeza katika hatua ya kuwawezesha Akinamama kielimu na Kiuchumi.

Ametoa wito kwa Serikali na Mashirika yasiyo ya kiserikali , vyombo vya Habari kuendelea kutoka Elimu na kuhamasisha Wanawake kujitokeza na kuanzisha Biashara mbalimbali bila woga na kujipatia kipato halali na kupiga hatua katika maendeleo ya familia na kubadili mwelekeo na mawazo ya kutengwa ama kunyanyasika.




Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items