Samatta amechaguliwa kwenye kikosi bora cha wiki cha UEFA

Kikosi bora cha wiki cha UEFA Europa League

Mshambuliaji wa timu ya RC Genk na nahodha wa Taifa stars, Mbwana Samatta amechaguliwa kwenye kikosi bora cha wiki cha UEFA Europe legue.

Samatta ametajwa katika kikosi bora cha wiki cha UEFA Europa League kwa mara ya kwanza katika historia lakini ametajwa pia na staa  mwenzake wa KRC Genk ambaye pia ni nahodha wao msaidizi wa Genk Pozuelo na mchezaji mwenzao Malinovskiy.

Jina la Samatta linakuwa ni miongoni mwa majina 11 kutoka katika baadhi ya timu 16 ambazo zina zaidi ya jumla ya wachezaji 176, waliyoonekana kufanya vizuri katika usiku wa round ya kwanza wa Europa League hatua ya 16 bora, kwa upande wa Man United staa wao Henrikh Mkhitaryan ndio katajwa katika list hiyo.
Mpya zaidi Nzee zaidi