Vijana CCM wajitokeza kwa wingi ubunge wa EALA

 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama cha mapinduzi , Humphrey Polepole amesema hadi kufikia jana Machi 24, wanachama wa CCM waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania ubunge wa Afrika Mashariki walikuwa 452.

Katika zoezi hilo la kuchukua fomu vijana wengi wa CCM wameonekana kuchangamkia nafasi hiyo ya ubunge wa EALA akiwemo aliyekuwa miss Tanzania wa zamani Basila Mwanukuzi,  kada mkereketwa Seki Boniventure Kasuga na wengine wengi.

Huu ni mchakato wa ndani wa chama hicho ili kupata wawakilishi na Ndugu Humphrey Polepole amesisitiza uadilifu.

"Tumesisitiza tena rushwa na vitendo vyote vinavyokwenda kinyume na kanuni za uchaguzi na uongozi havitavumiliwa, wote watakaoshiriki matendo hayo vikao vya chama vitayaondoa majina yao". Alisema Polepole

Chama cha CCM kinatakiwa kutoa wawakilishi 6 watakaokwenda kuwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika (EALA)

Basila Mwanukuzi na Seki Kasuga
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Ujuwe Ugonjwa wa Busha

Kilimo cha Bamia