Wanaohifadhi wahamiaji haramu kukiona

Manispaa ya Kinondoni  imesema mwananchi atakayekamatwa kwa kosa la kumuhifadhi mhamiaji haramu atapata adhabu sawa na mhamiaji aliyemhifadhi.

Kauli hiyo imetolewa na Inspekta Msaidizi wa Manispaa hiyo, Joyce Darushi wakati akijibu kero za wananchi kuhusu  kuwapo kwa wakazi kutoka Malawi.

Darushi amesema  kuwa sheria zipo wazi kuwa ni kosa kumuhifadhi mhamiaji haramu na kwamba atakayekiuka atapata adhabu sawa na mhamiaji huyo.

"Tuna habari ya kuwapo kwa wahamiaji hao wanaofichwa na wakazi, operesheni inayokuja  na hatapona mtu," amesema Darushi.
Mpya zaidi Nzee zaidi