Habari njema kumuhusu Msanii Beka


Msanii Beka Ibrozama ambaye pia ni kiongozi wa band iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa Spidoch Band ambayo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 29/4/2017 amefunguka na kusema sasa amerudi rasmi kwenye muziki. 

Akiongea ndani ya eNewz Beka amesema uzinduzi wa band hiyo utaanza saa mbili usiku katika Club ya Nextdoor Masaki ambapo VIP ni laki moja na Normal yani kawaida ni elfu 20 pia  amesisitiza mashabiki pamoja na wadau wa muziki kujitokeza kwa wingi kwa kuwa hiyo itakuwa show yao ya kwanza tangu kuanzishwa kwa band hiyo.

Hata hivyo Beka amesema band yake imetumia muda mrefu sana kufanya mazoezi na kuhakikisha kwamba ni band ambayo itafanya show mpaka za kimataifa  kwa kuwa wametumia muda mwingi kwenye mazoezi ya  band ili kuiandaa na mpaka sasa ni  zaidi ya  miaka sita.

Pia Beka amewaambia mashabiki zake kwamba alipotea kwa muda mrefu kimuziki kwa kuwa aliamua kujitolea muda wake wote kwaajili ya kuandaa band yake na kwa sasa amerudi rasmi kwenye muziki na mashabiki zake wasubiri kupata mziki mzuri kutoka kwake.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia