Mwanamke akutwa amekufa gesti

Songea. Mkazi wa Newala Mkoani Mtwara Asha Rais (41) amekutwa akiwa amefariki dunia kwenye nyumba ya kulala wageni ambayo ipo karibu na uwanja wa michezo wa timu ya Majimaji katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.

Akizungumza na Mwananchi leo Ofisini, kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Zuberi Mwombeji amesema kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 12:45 jioni katika k nyumba ya kulala wageni iitwayo Salama, Kata ya Mfaranyaki.

Mwombeji amesema kuwa inadaiwa siku hiyo kabla ya tukio Asha alikuwa amepanga chumba katika nyumba hiyo ya kulala wageni na baadaye wahudumu walimkuta akiwa amefariki dunia.

Kwa mujibu wa Kamanda Mwombeji, marehemu alikuwa safarini akitokea Newala, kuelekea Songea na alilazimika kulala katika gesti hiyo ili aendelee na safari siku inayofuata.

“Wahudumu wa gesti walimuona yupo kimya tangu aingie ndani hajatoka, ndipo walipoamua kuwaita polisi  ambao waliuvunja mlango na kumkuta Asha akiwa amefariki lakini hana jeraha lolote.” amesema
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia