Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Jumanne ametangaza kutoa takriban dola milioni 8 sawia na shilingi milioni 800 kwa raia waliolazimika kuhama maeneo mengine ya nchi hiyo kufuatia ghasia baada ya uhaguzi mwaka 2007.
Raia wa Kenya hasa kanda ya kuisni Magharibi mwa Kenya ndio walioathirika zaidi na ghasia hizo.
Rais Uhuru alikuwa anaongea katika kampeni zake za uchaguzi unaotarajiwa mwezi Agosti mwaka 2017.
Uhuru alitoa takriban shilingi milioni 348 kwa maelfu ya waliokosa makao kipindi hicho cha ghasia baada ya uchaguzi kati ya mwaka 2007 na 2008.
Fedha milioni 472 sarafu ya Kenya zilizobakia zitatolewa kwa waathirika wengine katika kaunti ya Nyamira na Kisii hapo siku ya Jumatano.
Rais Uhuru Kenyatta ametoa wito wa amani hasa baada ya Uchaguzi mkuu kumalizika mwezi Agosti.