Habari njema kutoka bodi ya mikopo elimu ya juu

Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Dk. Cosmas Mwaisobwa, alisema hayo jana alipokuwa akijibu maswali ya baadhi ya wateja waliotembelea banda la bodi hiyo kwenye Maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara, yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.

“Tunakamilisha mwongozo wa utoaji mikopo kwa mwaka ujao wa masomo na tumepanga kabla ya mwisho wa mwezi huu tuwe tumetangaza na tumefunga mtandao wetu ili waombaji wenye sifa waombe,” alisema.

Dk. Mwaisobwa amewataka waombaji wa mikopo watarajiwa wawe watulivu na kufuatilia kwa karibu vyombo vya habari na tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz) ambayo huwa na kiunganishi (link) cha mfumo wa kuombea mkopo.

Awali, katika maonyesho hayo, baadhi ya wananchi wanaotarajia kuomba mikopo ya elimu ya juu wamepata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali yakiwemo tarehe ambayo Bodi itaanza kupokea maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018.

Katika ufafanuzi wake kutokana na maswali hayo, Dk. Mwaisobwa alisema sheria iliyoanzisha HESLB, pamoja na mambo mengine, inamtaka mnufaika kuanza kurejesha mkopo wake miezi 24 baada ya kuhitimu masomo.

Pia alisema sheria hiyo inamtaka mwajiri yeyote kuwasilisha HESLB majina ya waajiriwa wake wote ambao ni wahitimu vya taasisi za elimu ya juu ndani ya siku 28 baada ya kuwaajiri na Bodi itamjulisha kama ni wanufaika au hapana pamoja na utaratibu na kiwango cha kumkata mnufaika.  
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia