Viongozi wa mataifa 19 katika mkutano wa mataifa tajiri duniani G20 unaofanyika nchini Ujerumani wameweka upya ahadi yao ya kuidhinisha makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya tabia nchi , licha ya Marekani kujiondoa.
Tofauti miongoni mwa viongozi zilionekana katika siku ya miwsho mjini Hamburg lakini hatimaye makubaliano yaliafikiwa.
Mkutano huo ulitambua hatua ya Marekani ya kujiondoa katika makubaliano ya Paris bila kukandamiza juhudi za mataifa mengine.
Makubaliano hayo yaliafikiwa baada ya maandamano ya ghasia katika mji ulioandaa mkutano huo.
Makubaliano hayo ya pamoja yaliotolewa Leo Jumamosi yalisema: Tunatambua hatua ya Marekani kujiondoa kutoka kwa makubaliano ya Paris.
Hatahivyo ,viongozi wa mataifa mengine ya G20 walikubaliana kwamba makubaliano hayo hayaweza kubadilishwa ili kuthibitisha mapatano hayo.
