Bawacha Watoa Msaada kwa Watoto Yatima

Baraza la Wanawake Chadema mkoa wa Dar es Salaam (Bawacha), wametoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha  kulelea watoto yatima, Yatima Group Trust Fund.

Msaada huo wa mifuko 35 ya saruji, sukari kilo 25, unga kilo 50, sabuni za maji, juice na mafuta ya kupikia ndoo moja ya lita 20.

Msaada huo umetolewa leo(Jumapili) ikiwa ni sehemu ya sherehe ya kuazimisha miaka 25 ya Chadema  na wenye thamani ya sh 2 milioni.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo kwa watoto yatima Mwenyekiti wa maandalizi ya sherehe hizo mkoa wa Dar es Salaam, Magreth Mugyabuso amesema Bawacha inathamini watu wenye mahitaji maalumu hivyo kutoa msaada kwa vituo vyote ndani ya mkoa na tayari walishafanya katika wilaya nyingine.

"Wanawake ndio msingi wa kulea jamii kwa ujumla hivyo kama Bawacha tumeguswa na maisha ya watoto hawa na hata wazee ambao wanauhitaji wa kupatiwa msaada ili kujihisi ni miongoni mwa watanzania wengine, "amesema Mugyabuso.

Mkurugenzi wa kituo hicho YGTF, Winfrida Lubanza amesema wanashukuru wanawake wa Chadema kwa kuguswa kutoa msaada huo.

" Ni wageni wa kwanza wakubwa tangu mwaka huu uanze na nafarijika kuwa watoto hawa siwalei peke yangu bali jamii kwa ujumla kwa wanaguswa na kuendelea kutoa kwa Moyo, "amesema Lubanza.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia