KOCHA WA AZAM FC ARISTICA CIOABA.
Azam na Simba zote zina pointi 19 huku wekundu wa Msimbazi wakiwa juu kwa tofauti ya mabao ya kushinda na kufungwa.
Akizungumza na gazeti hili, Cioaba, alisema kuwa wanafahamu mchezo huo wa leo wa ugenini utakuwa mgumu lakini ni lazima wapambane ili kuendelea kufukuzana na Simba kileleni.
“hatuangalii matokeo ya wapinzani wetu kwenye msimamo, tunataka kuendelea kupigania kukaa kileleni, tutapambana na wachezaji wangu wanafahamu nini tunatakiwa kufanya,” alisema Cioaba.
Aidha, alisema kuwa ugumu pekee anaofikiria kwenye mchezo wa leo ni juu ya ubovu wa uwanja wa Sabasaba watakaoutumia leo.
“Ubora wa uwanja unachangia kwenye matokeo, lakini hiyo ni changamoto ambayo ni lazima tukabiliane nayo,” alisema Cioaba.
Mchezo huo wa leo unatarajiwa kuwa mgumu na wenye upinzani hasa kutokana na Njombe Mji kuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani ambao mara nyingi wamekuwa wakicheza vizuri na kuonyesha upinzani dhidi ya timu za Dar es Salaam.
