Maafisa wanne wa polisi kuchukuliwa hatua kwa mauaji ya mtoto wa miezi 6

Maafisa wanne wa juu huko Kisumu Kenya wanatarajiwa kuchukuliwa hatua za kisheria kwa mauaji ya mtoto wa miezi 6 Samantha Pendo kilichotokea wakati wa vurugu za uchaguzi mwezi wa nane

Mwendesha mashtaka mkuu wa serikali Keriako Tobiko ameagiza Jeshi la polisi kuwachukulia hatua maafisa waandamizi na pia kuagiza uchunguzi wa wa Stephanie Moraa Gisemba mwenye umri wa miaka 8 huko Nairobi uanze

Jeshi la polisi pia litatakiwa kuwalipa fidia familia zilizoathirika

Watoto hao waliuawa na polisi waliokuwa wameagizwa kuzuia maandamano huko Mathare na Nyalenda

Hii inakuja siku chache baada ya Mamlaka Huru ya Kuchunguza Utendaji wa Polisi kutangaza kuwa imekamilisha uchunguzi juu ya mauaji 12 yaliyofanywa na polisi na kupeleka mafaili yake kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia