MSHAMBULIAJI WA SIMBA, EMMANUEL OKWI.
Magoli hayo mawili aliyofunga katika ushindi wa mabao 4-0 yamemfanya sasa mshambuliaji huyo raia wa Uganda kufikisha mabao 12 kwenye ligi msimu huu na kuongoza kwa idadi kubwa ya mabao.
"Nawashukuru mashabiki wanaoendelea kutusapoti na kututia moyo katika kila mchezo, mabao haya niliyoyafunga leo ni kwa ajili yao," alisema Okwi.
"Tutaendelea kupambana kuhakikisha tunafikia malengo yetu ya kutwaa ubingwa msimu huu, na hilo linawezekana," aliongeza kusema Okwi.
Mbao hayo ya jana yanamfanya Okwi kumuacha kwa mabao manne mfungaji anayemfuatia ambaye ni mshambuliaji wa Mbao FC, Habib Kayombo.
Okwi anaonekana kuwa hatari pindi Simba inapocheza jijini Dar es Salaam, lakini mpaka sasa hajaifungia timu hiyo bao lolote nje ya viwanja vya Dar es Salaam.
Hiyo inamaanisha mabao yote 12 ameyafunga kwenye viwanja vya Uhuru na Uwanja wa Taifa.
